43Bwana akamwambia Mose na Aroni, “Haya ndiyo masharti kwa ajili ya Pasaka: “Mgeni hataruhusiwa kula Pasaka.
44Mtumwa yeyote ambaye mmemnunua aweza kuila kama mmemtahiri,
45lakini kibarua yeyote au msafiri haruhusiwi kula.
46“Sharti iliwe ndani ya nyumba; msichukue nyama yoyote nje ya nyumba hiyo. Msiuvunje mfupa wowote.
47Jumuiya yote ya Israeli ni lazima waiadhimishe Pasaka hiyo.