4Kisha ingiza kinara cha taa na uweke taa zake juu yake.
5Weka madhabahu ya dhahabu ya kufukizia uvumba mbele ya Sanduku la Ushuhuda kisha uweke pazia kwenye lango la Maskani ya Mungu.
6“Weka madhabahu ya sadaka za kuteketezwa mbele ya lango la Maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania;
7weka sinia kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, na uweke maji ndani yake.
8Fanyiza ua kuzunguka maskani na uweke pazia penye ingilio la ua.