20Hawa ndio walikuwa wana wa Seiri, Mhori, waliokuwa wakiishi katika nchi ile: Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana,
21Dishoni, Eseri na Dishani. Hawa ndio wana wa Seiri huko Edomu waliokuwa wakuu kwa Wahori.
22Wana wa Lotani walikuwa: Hori na Homamu. Timna alikuwa dada yake Lotani.
23Wana wa Shobali walikuwa: Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu.
24Wana wa Sibeoni walikuwa: Aiya na Ana. Huyu Ana ndiye aligundua chemchemi ya maji moto jangwani alipokuwa akichunga punda za Sibeoni baba yake.