Mwanzo 9

Alipokunywa huo mvinyo wake akalewa na akalala uchi kwenye hema lake.

Genesis 9:21 (UKJV) And he drank of the wine, and was drunken; and he was uncovered within his tent.

19Hawa ndio waliokuwa wana watatu wa Noa, kutokana nao watu walienea katika dunia.

20Noa akawa mkulima, akawa mtu wa kwanza kupanda mizabibu.

21Alipokunywa huo mvinyo wake akalewa na akalala uchi kwenye hema lake.

22Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake na kuwaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.

23Lakini Shemu na Yafethi wakachukua nguo wakaitanda mabegani mwao wote wawili, kisha wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao. Nyuso zao zilielekea upande mwingine ili wasiuone uchi wa baba yao.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.