Isaya 1

“Mtaaibika kwa sababu ya hiyo mialoni ambayo mlifurahia, mtafadhaika kwa sababu ya bustani mlizozichagua.

Isaiah 1:29 (UKJV) For they shall be ashamed of the oaks which all of you have desired, and all of you shall be confounded for the gardens that all of you have chosen.

27Sayuni itakombolewa kwa haki, wale waliomo ndani yake waliotubu kwa uaminifu.

28Lakini waasi na wenye dhambi wote wataangamizwa, nao wanaomwacha Bwana wataangamia.

29“Mtaaibika kwa sababu ya hiyo mialoni ambayo mlifurahia, mtafadhaika kwa sababu ya bustani mlizozichagua.

30Mtakuwa kama mwaloni wenye majani yanayonyauka, kama bustani isiyokuwa na maji.

31Mtu mwenye nguvu atatoweka kama majani makavu yawakayo moto, na kazi yake kama cheche ya moto; vyote vitaungua pamoja, wala hakuna wa kuuzima huo moto.”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.