12Bwana Mwenye Nguvu Zote anayo siku aliyoiweka akiba kwa wote wenye kujivuna na wenye kiburi, kwa wote wanaojikweza (nao watanyenyekezwa),
13kwa mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu sana, na mialoni yote ya Bashani,
14kwa milima yote mirefu na vilima vyote vilivyoinuka,
15kwa kila mnara ulio mrefu sana na kila ukuta wenye ngome,
16kwa kila meli ya biashara, na kila chombo cha baharini cha fahari.