1Katika siku ile, wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda: Tuna mji ulio na nguvu, Mungu huufanya wokovu kuwa kuta zake na maboma yake.
2Fungua malango ili taifa lenye haki lipate kuingia, taifa lile lidumishalo imani.
3Utamlinda katika amani kamilifu yeye ambaye moyo wake ni thabiti kwa sababu anakutumaini wewe.
4Mtumaini Bwana milele, kwa kuwa Bwana, Bwana, ni Mwamba wa milele.
5Huwashusha wale wajikwezao, huushusha chini mji wenye kiburi, huushusha hadi ardhini na kuutupa chini mavumbini.