3Utamlinda katika amani kamilifu yeye ambaye moyo wake ni thabiti kwa sababu anakutumaini wewe.
4Mtumaini Bwana milele, kwa kuwa Bwana, Bwana, ni Mwamba wa milele.
5Huwashusha wale wajikwezao, huushusha chini mji wenye kiburi, huushusha hadi ardhini na kuutupa chini mavumbini.
6Miguu huukanyaga chini, miguu ya hao walioonewa, hatua za hao maskini.
7Mapito ya wenye haki yamenyooka. Ewe uliye Mwenye Haki, waisawazisha njia ya mtu mnyofu.