1Jangwa na nchi kame vitafurahi; nyika itashangilia na kuchanua maua. Kama waridi,
2litachanua maua, litashangilia sana na kupaza sauti kwa furaha. Litapewa utukufu wa Lebanoni, fahari ya Karmeli na Sharoni; wataona utukufu wa Bwana, fahari ya Mungu wetu.
3Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu, yafanyeni imara magoti yaliyolegea,
4waambieni wale wenye mioyo ya hofu, “Kuweni hodari, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja, pamoja na malipo ya Mungu, atakuja na kuwaokoa ninyi.”
5Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa na masikio ya viziwi yatazibuliwa.