Isaya 35

Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa na masikio ya viziwi yatazibuliwa.

Isaiah 35:5 (UKJV) Then the eyes of the blind shall be opened, and the ears of the deaf shall be unstopped.

3Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu, yafanyeni imara magoti yaliyolegea,

4waambieni wale wenye mioyo ya hofu, “Kuweni hodari, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja, pamoja na malipo ya Mungu, atakuja na kuwaokoa ninyi.”

5Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa na masikio ya viziwi yatazibuliwa.

6Ndipo kilema atarukaruka kama kulungu, nao ulimi wa aliye bubu utapaza sauti kwa shangwe. Maji yatatiririka kwa kasi katika nyika, na vijito katika jangwa.

7Mchanga wa moto utakuwa bwawa la maji, ardhi yenye kiu itabubujika chemchemi. Maskani ya mbweha walikolala hapo awali patamea majani, matete na mafunjo.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.