Isaya 40

Huwapa nguvu waliolegea na huongeza nguvu za wadhaifu.

Isaiah 40:29 (UKJV) He gives power to the faint; and to them that have no might he increases strength.

27Kwa nini unasema, ee Yakobo, nanyi ee Israeli, kulalamika, “Njia yangu imefichwa Bwana asiione, Mungu wangu hajali shauri langu?”

28Je wewe, hufahamu? Je wewe, hujasikia? Bwana ni Mungu wa milele, Muumba wa miisho ya dunia. Hatachoka wala kulegea, wala hakuna hata mmoja awezaye kuupima ufahamu wake.

29Huwapa nguvu waliolegea na huongeza nguvu za wadhaifu.

30Hata vijana huchoka na kulegea, nao vijana wanaume hujikwaa na kuanguka,

31bali wale wamtumainio Bwana atafanya upya nguvu zao. Watapaa juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio wala hawatachoka, watatembea kwa miguu wala hawatazimia.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.