Isaya 57

nikiumba sifa midomoni ya waombolezaji katika Israeli. Amani, amani, kwa wale walio mbali na kwa wale walio karibu,” asema Bwana. “Nami nitawaponya.”

Isaiah 57:19 (UKJV) I create the fruit of the lips; Peace, peace to him that is far off, and to him that is near, says the LORD; and I will heal him.

17Nilighadhibika na tamaa yake ya dhambi; nilimwadhibu, nikauficha uso wangu kwa hasira, na bado aliendelea katika njia zake za tamaa.

18Nimeziona njia zake, lakini nitamponya, nitamwongoza na kumrudishia upya faraja,

19nikiumba sifa midomoni ya waombolezaji katika Israeli. Amani, amani, kwa wale walio mbali na kwa wale walio karibu,” asema Bwana. “Nami nitawaponya.”

20Bali waovu ni kama bahari ichafukayo, ambayo haiwezi kutulia, mawimbi yake hutupa takataka na matope.

21Mungu wangu asema, “Hakuna amani kwa waovu.”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.