20Moabu amefedheheshwa, kwa kuwa amevunjavunjwa. Lieni kwa huzuni na kupiga kelele! Tangazeni kando ya Arnoni kwamba Moabu ameangamizwa.
21Hukumu imefika kwenye uwanda wa juu: katika Holoni, Yahasa na Mefaathi,
22katika Diboni, Nebo na Beth-Diblathaimu,
23katika Kiriathaimu, Beth-Gamuli na Beth-Meoni,
24katika Keriothi na Bosra; kwa miji yote ya Moabu, iliyoko mbali na karibu.