23katika Kiriathaimu, Beth-Gamuli na Beth-Meoni,
24katika Keriothi na Bosra; kwa miji yote ya Moabu, iliyoko mbali na karibu.
25Pembe ya Moabu imekatwa, mkono wake umevunjwa,” asema Bwana.
26“Mlevye, kwa kuwa amemdharau Bwana. Moabu na agaegae katika matapishi yake, yeye na awe kitu cha dhihaka.
27Je, Israeli hakuwa kitu chako cha kudhihakiwa? Je, alikamatwa miongoni mwa wezi, kiasi cha kutikisa kichwa chako kwa dharau kila mara unapozungumza juu yake?