Yeremia 48

Moabu ataangamizwa kama taifa kwa sababu amemdharau Bwana.

Jeremiah 48:42 (UKJV) And Moab shall be destroyed from being a people, because he has magnified himself against the LORD.

40Hili ndilo asemalo Bwana: “Tazama! Tai anashuka chini, akitanda mabawa yake juu ya Moabu.

41Miji itatekwa na ngome zake zitatwaliwa. Katika siku hiyo, mioyo ya mashujaa wa Moabu itakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wa kuzaa.

42Moabu ataangamizwa kama taifa kwa sababu amemdharau Bwana.

43Hofu kuu, shimo na mtego vinawangojea, enyi watu wa Moabu,” asema Bwana.

44“Yeyote atakayeikimbia hiyo hofu kuu ataanguka ndani ya shimo, yeyote atakayepanda kutoka shimoni, atanaswa katika mtego, kwa sababu nitaletea Moabu mwaka wa adhabu yake,” asema Bwana.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.