3Sikiliza kilio kutoka Horonaimu, kilio cha maangamizi makuu na uharibifu.
4Moabu utavunjwa, wadogo wake watapiga kelele.
5Wanapanda kwenda njia ya kuelekea Luhithi, wakilia kwa uchungu wanapotembea, kwenye njia inayoshuka kwenda Horonaimu, kilio cha uchungu kwa ajili ya uharibifu kinasikika.
6Kimbieni! Okoeni maisha yenu, kuweni kama kichaka jangwani.
7Kwa kuwa mmetumainia matendo yenu na mali zenu, ninyi pia mtachukuliwa mateka, naye Kemoshi atakwenda uhamishoni, pamoja na makuhani wake na maafisa wake.