16Hakika utaisahau taabu yako, utaikumbuka tu kama maji yaliyokwisha kupita.
17Maisha yako yatangʼaa kuliko adhuhuri, nalo giza litakuwa kama alfajiri.
18Utakuwa salama, kwa kuwa lipo tumaini; utatazama pande zote na kupumzika kwa salama.
19Utalala, wala hakuna atakayekuogofya, naam, wengi watajipendekeza kwako.
20Bali macho ya waovu hayataona, wokovu utawaepuka; tarajio lao litakuwa ni hangaiko la mtu anayekata roho.”