12Maneno yenu ni mithali za majivu; utetezi wenu ni ngome za udongo wa mfinyanzi.
13“Nyamazeni kimya nipate kusema; kisha na yanipate yatakayonipata.
14Kwa nini nijiweke mwenyewe kwenye hatari na kuyaweka maisha yangu mikononi mwangu?
15Ingawa ataniua, bado nitamtumaini; hakika nitazitetea njia zangu mbele zake.
16Naam, hili litanigeukia kuwa wokovu wangu, kwa maana hakuna mtu asiyemcha Mungu atakayethubutu kuja mbele yake!