19(wakati ambao wao peke yao ndio walipewa nchi, hakuna mgeni aliyepita miongoni mwao):
20Mtu mwovu siku zake zote hupata mateso, miaka yote aliwekewa mkorofi.
21Sauti za kutisha hujaa masikioni mwake; katika kufanikiwa kwake, wanyangʼanyi humshambulia.
22Hukata tamaa kuokoka gizani; amewekwa kwa ajili ya upanga.
23Hutangatanga, akitafuta chakula; anajua kwamba siku ya giza iko karibu.