20Mtu mwovu siku zake zote hupata mateso, miaka yote aliwekewa mkorofi.
21Sauti za kutisha hujaa masikioni mwake; katika kufanikiwa kwake, wanyangʼanyi humshambulia.
22Hukata tamaa kuokoka gizani; amewekwa kwa ajili ya upanga.
23Hutangatanga, akitafuta chakula; anajua kwamba siku ya giza iko karibu.
24Taabu na maumivu makuu vinamtia hofu; humshinda kama mfalme aliye tayari kwa vita,