22Hukata tamaa kuokoka gizani; amewekwa kwa ajili ya upanga.
23Hutangatanga, akitafuta chakula; anajua kwamba siku ya giza iko karibu.
24Taabu na maumivu makuu vinamtia hofu; humshinda kama mfalme aliye tayari kwa vita,
25kwa sababu amemkunjia Mungu ngumi yake na kujigamba dhidi ya Mwenyezi,
26kwa kiburi akishambulia dhidi ya Mungu akiwa na ngao nene, iliyo imara.