9Tanzi litamkamata kwenye kisigino; mtego utamshikilia kwa nguvu.
10Kitanzi kimefichwa ardhini kwa ajili yake; mtego uko kwenye njia yake.
11Vitisho vimemtia hofu kila upande, na adui zake humwandama kila hatua.
12Janga linamwonea shauku; maafa yako tayari kwa ajili yake aangukapo.
13Nayo yatakula sehemu ya ngozi yake; mzaliwa wa kwanza wa mauti atakula maungo yake.