11Vitisho vimemtia hofu kila upande, na adui zake humwandama kila hatua.
12Janga linamwonea shauku; maafa yako tayari kwa ajili yake aangukapo.
13Nayo yatakula sehemu ya ngozi yake; mzaliwa wa kwanza wa mauti atakula maungo yake.
14Atangʼolewa kutoka usalama wa hema lake, na kupelekwa kwa mfalme wa vitisho.
15Moto utakaa katika hema lake; moto wa kiberiti utamwagwa juu ya makao yake.