24Ijapokuwa aikimbia silaha ya chuma, mshale wa shaba utamchoma.
25Atauchomoa katika mgongo wake, ncha ingʼaayo kutoka ini lake. Vitisho vitakuja juu yake;
26giza nene linavizia hazina zake. Moto usiopepewa na mtu utamteketeza, na kuangamiza yaliyosalia nyumbani mwake.
27Mbingu zitaweka wazi hatia yake, nayo nchi itainuka kinyume chake.
28Mafuriko yataichukua nyumba yake, maji yaendayo kasi katika siku ya ghadhabu ya Mungu.