22Katikati ya wingi wa ustawi wake, dhiki itampata; taabu itamjia kwa nguvu zote.
23Atakapokuwa amelijaza tumbo lake, Mungu ataionyesha ghadhabu kali dhidi yake, na kumnyeshea mapigo juu yake.
24Ijapokuwa aikimbia silaha ya chuma, mshale wa shaba utamchoma.
25Atauchomoa katika mgongo wake, ncha ingʼaayo kutoka ini lake. Vitisho vitakuja juu yake;
26giza nene linavizia hazina zake. Moto usiopepewa na mtu utamteketeza, na kuangamiza yaliyosalia nyumbani mwake.