25ndipo Mwenyezi atakuwa dhahabu yako, naye atakuwa fedha yako iliyo bora.
26Hakika ndipo utakapojifurahisha kwa Mwenyezi, nawe utamwinulia Mungu uso wako.
27Utamwomba yeye, naye atakusikia, nawe utazitimiza nadhiri zako.
28Utakusudia jambo nalo litatendeka, nao mwanga utaangazia njia zako.
29Watu watakaposhushwa, nawe ukasema, ‘Wainue!’ ndipo atamwokoa aliyevunjika moyo.