24kama dhahabu yako ukiihesabu kama mavumbi, dhahabu yako ya Ofiri kama miamba ya mabondeni,
25ndipo Mwenyezi atakuwa dhahabu yako, naye atakuwa fedha yako iliyo bora.
26Hakika ndipo utakapojifurahisha kwa Mwenyezi, nawe utamwinulia Mungu uso wako.
27Utamwomba yeye, naye atakusikia, nawe utazitimiza nadhiri zako.
28Utakusudia jambo nalo litatendeka, nao mwanga utaangazia njia zako.