22Uyapokee mafundisho toka kinywani mwake, na maneno yake uyaweke moyoni mwako.
23Kama ukimrudia Mwenyezi, utarudishwa upya: Kama ukiuondoa uovu uwe mbali na hema lako,
24kama dhahabu yako ukiihesabu kama mavumbi, dhahabu yako ya Ofiri kama miamba ya mabondeni,
25ndipo Mwenyezi atakuwa dhahabu yako, naye atakuwa fedha yako iliyo bora.
26Hakika ndipo utakapojifurahisha kwa Mwenyezi, nawe utamwinulia Mungu uso wako.