3Laiti ningefahamu mahali pa kumwona; laiti ningeweza kwenda mahali akaapo!
4Ningeliweka shauri langu mbele zake, na kukijaza kinywa changu na hoja.
5Ningejua kwamba angenijibu nini, na kuelewa lile ambalo angelisema.
6Je, angenipinga kwa nguvu nyingi? La, asingenigandamiza.
7Hapo mtu mwadilifu angeweka shauri lake mbele zake, nami ningeokolewa milele na mhukumu wangu.