5Ningejua kwamba angenijibu nini, na kuelewa lile ambalo angelisema.
6Je, angenipinga kwa nguvu nyingi? La, asingenigandamiza.
7Hapo mtu mwadilifu angeweka shauri lake mbele zake, nami ningeokolewa milele na mhukumu wangu.
8“Lakini nikienda mashariki, hayupo; nikienda magharibi, simpati.
9Anapokuwa kazini pande za kaskazini, simwoni; akigeukia kusini, nako simwoni hata kidogo.