6Je, angenipinga kwa nguvu nyingi? La, asingenigandamiza.
7Hapo mtu mwadilifu angeweka shauri lake mbele zake, nami ningeokolewa milele na mhukumu wangu.
8“Lakini nikienda mashariki, hayupo; nikienda magharibi, simpati.
9Anapokuwa kazini pande za kaskazini, simwoni; akigeukia kusini, nako simwoni hata kidogo.
10Lakini anaijua njia niiendeayo; akiisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.