14Hata kama watoto wake watakuwa wengi kiasi gani, fungu lao ni kuuawa kwa upanga; wazao wake hawatakuwa kamwe na chakula cha kuwatosha.
15Tauni itawazika wale watakaonusurika miongoni mwao, nao wajane wao hawatawaombolezea.
16Ajapokusanya fedha nyingi kama mavumbi, na mavazi kama malundo ya udongo wa mfinyanzi,
17yale yote mtu mwovu aliyojiwekea akiba, mwenye haki atayavaa, naye asiye na hatia ataigawanya fedha yake.
18Nyumba aijengayo ni kama utando wa buibui, kama kibanda alichotengeneza mlinzi.