15Tauni itawazika wale watakaonusurika miongoni mwao, nao wajane wao hawatawaombolezea.
16Ajapokusanya fedha nyingi kama mavumbi, na mavazi kama malundo ya udongo wa mfinyanzi,
17yale yote mtu mwovu aliyojiwekea akiba, mwenye haki atayavaa, naye asiye na hatia ataigawanya fedha yake.
18Nyumba aijengayo ni kama utando wa buibui, kama kibanda alichotengeneza mlinzi.
19Yeye hulala akiwa tajiri, lakini ndiyo mara ya mwisho; afunguapo macho yake, yote yametoweka.