17yale yote mtu mwovu aliyojiwekea akiba, mwenye haki atayavaa, naye asiye na hatia ataigawanya fedha yake.
18Nyumba aijengayo ni kama utando wa buibui, kama kibanda alichotengeneza mlinzi.
19Yeye hulala akiwa tajiri, lakini ndiyo mara ya mwisho; afunguapo macho yake, yote yametoweka.
20Vitisho humjia kama mafuriko; dhoruba humkumba ghafula usiku.
21Upepo mkali wa mashariki humchukua, naye hutoweka; humzoa kutoka mahali pake.