19Yeye hulala akiwa tajiri, lakini ndiyo mara ya mwisho; afunguapo macho yake, yote yametoweka.
20Vitisho humjia kama mafuriko; dhoruba humkumba ghafula usiku.
21Upepo mkali wa mashariki humchukua, naye hutoweka; humzoa kutoka mahali pake.
22Humvurumisha bila huruma, huku akikimbia kasi kukwepa nguvu zake.
23Upepo humpigia makofi kwa dharau, na kumfukuza atoke mahali pake.