1“Kuna machimbo ya fedha, na mahali dhahabu isafishwapo.
2Chuma hupatikana ardhini, nayo shaba huyeyushwa kutoka mawe ya madini.
3Mwanadamu hukomesha giza; huyatafuta hadi sehemu iliyo mbali, kwa ajili ya kuchimbua mawe yenye madini katika giza jeusi sana.
4Huchimba shimo jembamba mbali na makao ya watu, mahali paliposahaulika na nyayo za wanadamu; mbali na wanadamu huningʼinia na kupembea kwa kamba.