11Yeyote aliyenisikia alinena mema juu yangu, nao walioniona walinisifu,
12kwa sababu nilimwokoa maskini aliyeomba msaada, naye yatima aliyekuwa hana wa kumsaidia.
13Mtu aliyekuwa karibu kufa alinibariki, nami niliufanya moyo wa mjane kuimba.
14Niliivaa haki kama vazi langu; uadilifu ulikuwa joho langu na kilemba changu.
15Nilikuwa macho ya kipofu na miguu kwa kiwete.