13Mtu aliyekuwa karibu kufa alinibariki, nami niliufanya moyo wa mjane kuimba.
14Niliivaa haki kama vazi langu; uadilifu ulikuwa joho langu na kilemba changu.
15Nilikuwa macho ya kipofu na miguu kwa kiwete.
16Nilikuwa baba kwa mhitaji; nilimtetea mgeni.
17Niliyavunja meno makali ya waovu, na kuwapokonya wahanga kwenye meno yao.