14Niliivaa haki kama vazi langu; uadilifu ulikuwa joho langu na kilemba changu.
15Nilikuwa macho ya kipofu na miguu kwa kiwete.
16Nilikuwa baba kwa mhitaji; nilimtetea mgeni.
17Niliyavunja meno makali ya waovu, na kuwapokonya wahanga kwenye meno yao.
18“Nikafikiri, ‘Nitafia katika nyumba yangu mwenyewe, nazo siku zangu zitakuwa nyingi kama chembechembe za mchanga.