16Nilikuwa baba kwa mhitaji; nilimtetea mgeni.
17Niliyavunja meno makali ya waovu, na kuwapokonya wahanga kwenye meno yao.
18“Nikafikiri, ‘Nitafia katika nyumba yangu mwenyewe, nazo siku zangu zitakuwa nyingi kama chembechembe za mchanga.
19Mizizi yangu itafika mpaka kwenye maji, nao umande utakaa juu ya matawi yangu usiku kucha.
20Utukufu wangu utabakia kuwa mpya ndani yangu, upinde wangu daima utaendelea kuwa mpya mkononi mwangu.’