15Nilikuwa macho ya kipofu na miguu kwa kiwete.
16Nilikuwa baba kwa mhitaji; nilimtetea mgeni.
17Niliyavunja meno makali ya waovu, na kuwapokonya wahanga kwenye meno yao.
18“Nikafikiri, ‘Nitafia katika nyumba yangu mwenyewe, nazo siku zangu zitakuwa nyingi kama chembechembe za mchanga.
19Mizizi yangu itafika mpaka kwenye maji, nao umande utakaa juu ya matawi yangu usiku kucha.