35(“Laiti kama angekuwepo mtu wa kunisikia! Tazama sasa ninatia sahihi kwenye utetezi wangu: Mwenyezi na anijibu; mshtaki wangu na aweke mashtaka yake kwenye maandishi.
36Hakika ningeyavaa begani mwangu, ningeyavaa kama taji.
37Ningempa hesabu ya kila hatua yangu, ningemwendea kama mwana wa mfalme.)
38“Kama nchi yangu inalia dhidi yangu, na mifereji yake yote imelowana kwa machozi,
39kama nimekula mazao yake bila malipo, au kuvunja mioyo ya wapangaji wake,