4Je, yeye hazioni njia zangu na kuihesabu kila hatua yangu?
5“Kama nimeishi katika uongo au mguu wangu umekimbilia udanganyifu,
6Mungu na anipime katika mizani za uaminifu, naye atajua kwamba sina hatia:
7kama hatua zangu zimepotoka kutoka kwenye njia, kama moyo wangu umeongozwa na macho yangu, au kama mikono yangu imetiwa unajisi,
8basi wengine na wale nilichokipanda, nayo yale yote niliyootesha na yangʼolewe.