21“Macho yake yanazitazama njia za wanadamu; anaona kila hatua yao.
22Hakuna mahali penye giza nene, wala uvuli mkubwa, ambapo watenda mabaya wanaweza kujificha.
23Mungu hana haja ya kumchunguza mtu sana, ili apate kuja mbele zake kwa hukumu.
24Bila kuuliza huwapondaponda wenye nguvu nyingi na kuwaweka wengine mahali pao.
25Kwa sababu huyaangalia matendo yao yote, huwaondoa usiku, nao wakaangamia.