24Bila kuuliza huwapondaponda wenye nguvu nyingi na kuwaweka wengine mahali pao.
25Kwa sababu huyaangalia matendo yao yote, huwaondoa usiku, nao wakaangamia.
26Anawaadhibu kwa ajili ya uovu wao mahali ambapo kila mmoja ataweza kuwaona,
27kwa sababu wameacha kumfuata Mungu, nao hawakuiheshimu njia yake hata moja.
28Wamesababisha kilio cha maskini kifike mbele zake, hivyo akasikia kilio cha wahitaji.