5“Ayubu anasema, ‘Mimi sina hatia, lakini Mungu ameninyima haki yangu.
6Ingawa niko sawa, ninaonekana mwongo; nami ingawa sina kosa, kidonda changu hakiponi.’
7Ni mtu gani aliye kama Ayubu, anywaye dharau kama maji?
8Ashirikianaye na watenda mabaya na kuchangamana na watu waovu.
9Kwa kuwa anasema, ‘Haimfaidi mwanadamu kitu chochote anapojitahidi kumpendeza Mungu.’