3Kwa kuwa sikio huyajaribu maneno kama vile ulimi uonjavyo chakula.
4Tujichagulie wenyewe yaliyo sawa, nasi tujifunze pamoja yaliyo mema.
5“Ayubu anasema, ‘Mimi sina hatia, lakini Mungu ameninyima haki yangu.
6Ingawa niko sawa, ninaonekana mwongo; nami ingawa sina kosa, kidonda changu hakiponi.’
7Ni mtu gani aliye kama Ayubu, anywaye dharau kama maji?