1Kisha Elihu akasema:
2“Sikieni maneno yangu, enyi watu wenye hekima; nisikilizeni mimi, ninyi watu wenye maarifa.
3Kwa kuwa sikio huyajaribu maneno kama vile ulimi uonjavyo chakula.
4Tujichagulie wenyewe yaliyo sawa, nasi tujifunze pamoja yaliyo mema.
5“Ayubu anasema, ‘Mimi sina hatia, lakini Mungu ameninyima haki yangu.