1Ndipo Elihu akasema:
2“Je, unadhani hili ni haki? Wewe unasema, ‘Nina haki mbele za Mungu.’
3Bado unamuuliza, ‘Ni faida gani nimepata, na imenifaidi nini kwa kutokutenda dhambi?’
4“Ningependa nikujibu wewe pamoja na marafiki zako walio pamoja nawe.
5Tazama juu mbinguni ukaone; yaangalie mawingu yaliyo juu sana juu yako.