8Wanyama hujificha; hubakia kwenye mapango yao.
9Dhoruba hutoka katika chumba chake, baridi hutoka katika upepo uendao kasi.
10Pumzi ya Mungu hutoa barafu, eneo kubwa la maji huganda.
11Huyasheheneza mawingu kwa maji, naye husambaza umeme wake wa radi kupitia hayo.
12Nayo mawingu huzungukazunguka pande zote kwa amri yake, juu ya uso wa dunia yote, kufanya lolote ayaamuruyo.